Monday 20 February 2017

Fid Q amtetea Profesa Jay baada ya Nash MC kumvunjia heshima (Audio)


Fid Q amefunguka baada ya siku chache zilizopita Nash MC kumkejeli rapper mkongwe nchini Profesa Jay. Jay alijibu kwa kudai kuna baadhi ya wasanii wa hip hop wana wivu kwa wengine ambao wamekuwa wakibadilisha muziki huo.






 Fid amesema wasanii wengi wamekuwa hawana elimu wala ujuzi wa hip hop ndio maana wanatokea watu wanaomvunjia heshima Prof Jay.
“Basically alichokisema Prof ni sawa kwamba hip hop ya siku hizi imekuwa ile ile kama baba sharubu, mama sharubu na mtoto sharubu. Ni vile tu ambavyo watu ambao wamebakia sasa hivi kwenye hip hop au jumuiya au hip hop community na kujivika kile cheo cha usemaji mkuu wa hip hop ni watu ambao hawana huo ujuzi na hiyo elimu ya hip hop yenyewe,” amesema Fd.
“Kwahiyo ndio maana tunakutana na hiyo mikangamo mingi mingi na tofauti tofauti kwamba mtu anaweza akatokea tu na kumdisrespect mtu kama Profesa Jay pasi na kuzingatia Profesa Jay kafanya nini katika hip hop hii ambayo watu wanaifanya sasa hivi,” ameongeza.


No comments:

Post a Comment