MBUNGE na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo(CHADEMA),
Tundu Lissu amemshukia Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe
akimtuhumu kuwa anataka kuharibu uchaguzi wao wa uraisi wa Chama cha
Wanasheria nchini (TLS) uliopangwa kufanyika Machi 18 mwaka huu.
Tundu Lissu ametaka ajumuishwe katika kesi ya Godfrey Sabato Wasonga
dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu uchaguzi wa TLS.
Akizungumza na wanahabari katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es
Salaam, Lissu amesema kuwa Mwakyembe anamtuhumu kuhusika kuwashawishi
wanasheria wawili waliofungua kesi mbili za kupinga kutokufanyila
uchaguzi huo kwa madai y akuwa uchaguzi huo unaingiliwa na masuala ya
kisiasa jambo ambalo lisu amelikataa akisema:
“Uchaguzi wetu wala hauhusiki na masuala ya kisiasa kwani sheria ya
Chama cha Wanasheria inavyovigezo vya kuzingatia na kuheshimu Katiba
yake na ndipo mwanachama anaruhusiwa kuomba uongozi pale anapokuwa
amekidhi vigezo.”
“Katika kugombea Urais wa Chama cha Wanasheria, mimi sijatumia vyeo
vyangu katika chama bali nimetumia vigezo vya kisheria ya chama cha
wanasheria ndio maana hata ukiangalia mwenzangu Laurence Masha naye
ametokea chadema.
“Kwa hiyo kama tungeingiza mambo ya siasa asingegombea yeye tukawa
wawili ndani ya chama, Mawakili waliofungua Kesi mkoa wa Dodoma na
wengine wa Dar es Salaam tutahakikisha tunanunua kesi hiyo kwa kwenda
Mahakamani kufungua kesi inayopinga kutokufanyika kwa uchaguzi huo, na
hilo tutalitekeleza kabla ya kufanyika kwa uchanguzi huo ili uchaguzi
wetu hauvurugiki,” Alisema Lissu
No comments:
Post a Comment