Thursday 16 February 2017

BIL NAS ;VIDEO YA MAZOEA IMENIGHARIMU KULIKO CHAF POZ ................




Rapper Bill Nas amesema kuwa kufanya video ya wimbo wake Mazoea Bongo badala ya Afrika Kusini, hakujaokoa gharama yoyote. Amedai kuwa licha ya video hiyo kufanyika nyumbani, imetumia gharama kubwa zaidi.

Amesema kile ambacho amekiokoa ni muda tu kwakuwa kama angesafiri kuna vitu vya nyumbani ambavyo angeviacha ‘pending.’
“Lakini kwenye suala la pesa video ya Mazoea imezidi gharama hadi video ya Chafu Pozi, imezidi sana. Labda kama ningeenda kuifanya kule gharama labda zingezidi sababu ilikuwa ni collaboration labda gharama za kumsafirisha Mwana FA makazi yake kule na vitu vingine, halafu tungesafiri na timu kubwa pia,” Bill Nas amemuambia mtangazaji wa Pride FM ya Mtwara, Eddy Msafi.
Video ya Mazoea imeongozwa na Msafiri.


No comments:

Post a Comment