Thursday 2 March 2017

Video Queen wa Harmonize Amvaa Harmorapa...!!!


VIDEO Queen aliyeuza nyago kwenye Ngoma ya Matatizo ya memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ aliyejitambulisha kwa jina la     amemvaa na kumpa makavu msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Omary Athuman ‘Harmorapa’ akimtaka kuacha kutumia jina la Harmonize kujitafutia umaarufu.
Akistorisha na Show Biz Xtra, Glady alifunguka kuwa anachukizwa na Harmorapa kumtumia Harmonize kupata jina kwani angeweza kutoka bila kutumia jina la Harmonize.
“Huyu Harmorapa ananichukiza sana. Hivi ni lazima atumie jina la Harmonize? Kiukweli sipendi kabisa staili yake hiyo na nikikutana naye nitampa makavu bila woga,” alisema Glady


No comments:

Post a Comment