Thursday 2 March 2017

Bashir amteua makamu wake kuwa waziri mkuu


Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, amemteuwa makamu wake wa rais Bakri Hassan Saleh kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.

Bwana Saleh ni mmoja wa mshirika wa karibu zaidi wa Bashir, na alihusika katika mapinduzi ya mwaka 1989 yaliyomleta mamlakani Omar Al Bashir.

Huku wakiwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa upinzani na jamii ya kimataifa, Bwana Mr Bashir amebuni cheo cha waziri mkuu, ambacho aliifutilia mbali mara tu baada ya kuingia uongozini kwa njia ya mapinduzi.


No comments:

Post a Comment