Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima,
amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani
nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na
mipasho ya kidunia.
Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza
kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo
kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.
Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani
anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba
wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.
Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali
sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya
kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote
kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.
Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za
kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee
anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi
vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es
Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa
watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi
kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment