Pamoja na kwamba Kocha Claudio Ranieri alionekana ameshindwa kabisa kuikomboa Leicester City kuporomoka daraja.
Taarifa
zinasema uhusiano wa karibu kati ya wachezaji na mmiliki wa timu hiyo
Vichai Srivaddhanaprabha ambaye ni mmiliki pia wa kampuni ya King Power
pia ulichangia kufeli kwa kocha huyo.
Imeelezwa,
baad ya Leicester kutwaa ubingwa wa England na kuwashitua watu wengi,
kuanzia hapo Srivaddhanaprabha alianza kuwa na urafiki wa karibu na
wachezaji.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wachezaji kuanza kupeleka maneno ya umbeya.
Lakini
baadhi yao walianza kuonyesha wao ni wakubwa kuliko kocha kwa kuwa pia
walikuwa na urafiki na mtoto wa mmiliki wa klabu hiyo.
Hali hiyo inaelezwa kuchangia kupunguza nidhamu na hofu kwa kocha na kusababisha kushuka kwa viwango vya wachezaji wengi.
Ingawa
kila mmoja amekuwa hataki kulizungumzia na mzigo anaangushiwa kocha
Ranieri kama ilivyo ada, lakini urafiki huo wa karibu wa
Srivaddhanaprabha na wachezaji pia pamoja na mwanaye umeelezwa kuchangia
kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment