Thursday 30 March 2017

MANARA ‘Ukiwatoa Dimond na King Kiba, Ajibu ndio anafata kwa kutoa burudani kwa jamii’

Afisa habari habari wa wekundu wa Msimbazi amemsifia mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib kwa kusema kwamba, ukitoa Ally Kiba na Dimond, Ajibu ndiye anaefuatia kwa kutoa burudani kwa jamii.
Manara ame-post umbe huo kwenye account yake ya Instagram akimuweka Ajib kwenye daraja la juu la watoa burudani hapa Bongo.
“Huyu Ajibu mpira unatii miguu yake, unamuogopa, ndio binadamu aliye hai nchini kwa sasa anayeburudisha jamii kuliko wote kando ya Dimond na Ally Kiba,” ndivyo unavyosomeka ujumbe wa Haji Manara kwenye account yake ya Instagram (hajismanara).
Ajib amekuwa akisifiwa na mashabiki pamoja na wadau wa soka kutokana na aina yake ya kuchezea na kumiliki mpira.


No comments:

Post a Comment