Wednesday 29 March 2017

MESSI AANDIKA UJUMBE HUU BAADA YA KUFUNGIWA NA FIFA KWA KOSA LA KUMTUKANA REFA


Moja kati ya stori zinazotawala katika mitandao ya kijamii kwa siku hizi mbili ni kuhusiana na staa wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi kufungiwa michezo minne na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Lionel Messi alifungiwa mechi nne na FIFA kwa kosa la kudaiwa kumtukana muamuzi wakati wa mchezo dhidi ya Chile uliyochezwa March 24 2017, baada ya kufungiwa Lionel Messi alikuwa kakaa kimya lakini leo mtandao wa bleacherreport umempata Lionel Messi.
“Maneno yangu hayakuwa yamemlenga moja kwa moja muamuzi msaidizi, kuna maneno ambayo yalikuwa yamesemwa kwangu mimi nilijisemea tu” >>> Lionel Messi
VIDEO INAYOMUONESHA LIONEL MESSI AKITOA LUGHA CHAFU




No comments:

Post a Comment