Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, waziri mpya wa habari utamaduni na michezo amekaribishwa wizarani na kuzungumzia mambo mbali mbali anayotarajia kuyafanya. Miongoni mwa mambo mengine, Mwakyembe amesema serikali duniani kote haziwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari, amedai atashirikiana nao.
Kuhusu sakata la mkuu wa mkoa kuvamia Clouds, Mwakyembe amedai japo ripoti hajaiona lakini yeye kama mwanasheria ni mwiko na hatapeleka kitu ambacho anaona hakijakamilika kwani kwa taarifa alizonazo kupitia vyombo vya habari ni kuwa taarifa yote inatokana na ushahidi wa mlalamikaji ambae ni Clouds lakini hakuna ushahidi wowote wa upande wa pili na wamekiri kuwa haukupatikani.
Amedai wanaheshimu sana kanuni za asili(Principles of natural justice) kwani mwanasheria yeyote lazima aheshimu kanuni hiyo, ameongeza kuwa mtu hawezi kuwa hakimu kwenye suala lake mwenyewe na yeye angekuwa active journalist asingeweza kulishughulikia. Pia kwa mujibu wake kanuni hio pia inasisitiza kusikilizwa upande wa pili hivyo hawezi kuwapelekea viongozi wake kitu ambacho kina upande mmoja kwa sababu itakuwa ni kuwapa kazi wao wautafute. Amesema kazi yake yeye sasa ni kutafuta upande wa pili na amedai ataupata tu.
Mwakyembe amesema jambo la Makonda sio kipaumbele kwenye wizara yake na hakuapa kwa ajili ya hilo suala peke yake na ni moja tu ya masuala mengi na hatayakwepa na atayaangalia. Amesisitiza yeye ni mwanasheria mkongwe na hawezi kufanya kosa la kupeleka taarifa ya upande mmoja viongozi wake wa juu kwani nao watamshangaa, pia hataunda kamati kwani kamati ni yeye mwenyewe na atakaa na wenzake.
Kwenye utamaduni amesema jambo kubwa ni kuendeleza lugha ya Kiswahili na amemshukuru Rais Maguful, amedai haiwezekani akaja mgeni akaongea kwa Kiingireza na sisi kutafsiriwa na ikifika zamu yetu bado tunajibu kwa Kiingereza. Amedai yeye amesoma Ujerumani na watu wanajivunia kwa lugha yao.
Amesema wajibu wao ni kuwapata vijana wanaojua lugha za kigeni na kuwalea kama wakishindwa kuwaajiri kama wizara. Amesema dunia nzima inajua nyumbani kwa Kiswahili ni Tanzania na Rais wa Jamhuri ameonyesha njia
No comments:
Post a Comment