Thursday, 30 March 2017

Shy-Rose Bhanji amechukizwa baada ya Jina lake kukatwa na Kamati Kuu ya CCM katika kinyang'anyiro cha ubunge Afrika Mashariki


Aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Shy-Rose Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika kinyang'anyiro cha kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma zilizopeleka jina lake kukatwa.

Licha ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza watu waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo waliopata kura nyingi zaidi.

"Ingawa jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. Ninawashukuru sana Wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura" aliandika Shy-Rose Bhanji


No comments:

Post a Comment