Tuesday 9 May 2017

JUMA KASEJA AZIMWAGIA CHOZI LA DAMU POINT TATU ZA YANGA....ASEMA HAYA.....

Golikipa wa Kagera Sugar Juma Kaseja amesema wanahitaji pointi za Yanga ili wasogee juu kwenye msimamo wa ligi ili wamalize katika nafasi ambazo walijipangia kama timu.
Kaseja ambaye amewahi kuitumikia Yanga amesema, Kagera Sugar imejiwekea malengo ya kumaliza katika nafasi tatu za juu.
“Nimejiunga na timu ikiwa raundi ya pili ya ligi, nimekuta imejiwekea malengo ya kumaliza katika nafasi nafasi tatu za juu kwa hiyo mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu kwa sababu tunahitaji pointi hizo ili usogee juu kwa sababu kwenye msimamo sasa hivi tumeshuka tupo nafasi ya nne,” amesema Kaseja golikipa wa zamani na nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
“Mpira hauna matokeo ya kukariri kwamba kwa sababu ulishinda raundi ya kwanza basi na raundi ya pili utashinda unaweza ukashinda leo lakini kesho ukapoteza. Sisi tumejipanga kwenda kucheza lakinin tunaamini mchezo utakuwa mgumu.”


No comments:

Post a Comment