Thursday 11 May 2017

KAULI YA ZITTO ''MAJUTA KUZALIWA TANZANIA'' YAMWEKA KATIKA UTATA HUU!! KAAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA



Jana usiku nilikwazika kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki ( EALA ). Kufuatia hasira hiyo nikaandika kuwa wakati mwengine unajiuliza Kama unastahili kuwa kwenye nchi ambayo umo Kama raia.

Haikuwa sahihi Kabisa Kwa Kiongozi wa ngazi yangu kujutia uraia wangu kwa sababu tu ya kundi la watu wachache kuamua kuchagua wawakilishi wetu kwenye taasisi za kimataifa bila kujali uwezo, uzoefu na weledi wa wawakilishi husika.

Ninajua hatua ya Sasa ya Mtangamano wa Afrika Mashariki Ni hatua muhimu mno kwani Ni hatua ya kuelekea Umoja wa Fedha ( Monetary Union). Ndio maana Mataifa mengine yamepeleka raia wao mahiri Kabisa. Rwanda wamepeleka Waziri Mkuu mstaafu na Mawaziri 2. Burundi imepeleka Waziri wake Wa Afrika Mashariki. Uganda imepeleka Mawaziri Wastaafu. Kenya imepeleka Wabunge wazoefu na Wafanyabiashara wakubwa. Hata mwanachama mpya Sudani ya Kusini imepeleka Waziri wa zamani, Spika wa Bunge wa zamani na Jenerali wa Jeshi.

Hasira za kuipenda nchi yangu Ndio zilinipelekea kuandika nilivyoandika.

Naomba radhi kwa andiko lile na ninalifuta. Hata hivyo, Wabunge wote wa vyama vyote wajue kuwa wameionea Nchi yetu. Wameweka maslahi ya vyama vyao na mahusiano yao mbele ya maslahi ya nchi yetu. Tanzania imepeleka 'amateurs' huko EALA. Huu ndio ukweli mchungu na lazima usemwe. Itabidi kuwa na program maalumu ya kuwafundisha wawakilishi wetu hawa. Kina Adam Kimbisa lazima wachukue jukumu hili bila kujali usumbufu wake.

Anyways! My country, Right or Wrong.

Zitto Kabwe (MB).


No comments:

Post a Comment