Sunday 7 May 2017

Rais Kenyatta wa Kenya amsimamisha shughuli kwaajil ya kuwaombea Wanafunzi 33 wa Tanzania Waliofariki Jana ......


Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenya amewaongoza raia wa nchi hiyo jana katika kuomboleza vifo vya wanafunzi 33 vilivyotokea Wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Kenyatta ambaye ni mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee, aliwaomba raia wa Kenya kusimama kwa dakika moja kuomboleza na kuwaombea wanafunzi 33, walimu 2 na dereva waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jana saa tatu asubuhi.

Rais Uhuru alitoa heshima hiyo alipokuwa katika moja ya mikutano yake ya hadhara nchini humo ambapo anatetea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.


No comments:

Post a Comment