Saturday 13 May 2017

RAMBIRAMBI KWA WAFIWA WA WANAFUNZI WA SHULE YA LUCK VICENT YAFANYIWA MCHEZO MCHAFU TAARIFA KAMILI HII HAPA



Familia za Wanafunzi, Waalimu/Dereva zilizopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya gari la shule ya Lucky Vincent huko Arusha zimepatiwa kila moja kiasi cha shilingi Milioni 3.6, (Pesa Zingine zilizotolewa zimetumika kugharamia gharama Zingine. Millions 60, 400,000) zipi?

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Arusha,jumla ya shilingi milioni 190 zimetumika kwenye gharama zote.

Kimahesabu jumla ya shilingi Milioni 129,600,000 ndizo walizopewa wafiwa kama Rambirambi baada ya matumizi mengine.Kiasi cha shilingi milioni 60,400,000 ndizo zilizotumika kwa matumizi mengineyo.

Swali langu moja tuu,
"Serikali ilitangaza itagharamia Mambo yoote ya Msiba mpaka kuzika, sasa hii ya kusema tena kiasi flani cha fedha ya Rambi rambi kilichotolewa kimetumika kwa mambo mengine ni yapi hayo? Ili kuondoa utata vichwani mwa wengi, ingependeza endapo yangetajwa.


No comments:

Post a Comment