Sunday 7 May 2017

UKWELI ULIOSHEHENI MACHUNGU YASIYOMEZEKA KUHUSU AJALI WALIYOIPATA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT UMEVUJA.....HUU HAPA....



Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina. 
Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo. 

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia. 

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia


3 comments:

  1. much respect to you my boy good investigation, you make me proud

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete