Wednesday 21 June 2017

HATIMAYE HARUNA NIYONZIMA KAKATA MZIZI WA FITNA BAADA YA KUIKANA YANAGA MCHNA KWEUPE KAULI YAKE!!!!!!!

Image result for niyonzima
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.

Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.

Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.

Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club.
21-06-2017.


No comments:

Post a Comment