Thursday 24 August 2017

AJALI MBAYA YA TRENI NA DALADALA MOROGORO YAUA WANAFUNZI NA WENGINE KUJERUIWA VIBAYA

Inasikitisha Ajali ya Treni na Daladala, Yaua Wanafunzi Mkoani Morogoro

Inasikitisha Ajal yai Treni na Daladala, Yaua Wanafunzi Mkoani Morogoro
Watu ambao idadi yake haijaweza kufahamika mara moja, wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa, baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria kugonga treni mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urich Matei, amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi na imehusisha gari aina ya daladala yenye amba za usajili T 438 ADR iliyokuwa inakwenda Mvumi kwenye njia panda inayoingilia treni ndipo ikagonga treni hiyo, na kuburuzwa takribani mita 200.

Kamanda Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni daladala kuingia kwenye njia ya treni bila kusimama ili kuangalia kama kuna treni inakuja, ndipo treni hiyo ikaburuza gari hiyo kwa umbali mrefu na kusababisha maafa hayo.

Idadi rasmi ya majeruhi bado haijafahamika rasmi mpaka sasa na majeruhi wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro
Read more »


Tuesday 22 August 2017

VITA YA TATU YAAMIA SIMBA YANGA NANI MBABE UKWELI UU HAPA




Kocha msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja ameibuka na kufunguka kuwa kwenye mchezo wa leo mbele ya Yanga hawana cha kupoteza huku wakiingia uwanjani wakiwa na lengo moja pekee la kushinda.

Mayanja aliyewahi kuinoa Kagera Sugar ya Kagera leo Jumatano atashirikiana na bosi wake, Joseph Omog raia wa Cameroon kusaka taji la Ngao ya Jamii kwa kuivaa Yanga, kwenye mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.


 Mayanja amesema kuwa kutokana na aina ya kikosi walichonacho ni imani yake kuwa wana kila sababu ya kuibuka na ushindi mbele ya Yanga na kuanza vizuri kabla ya msimu wa 2017/18.

“Tunawaza kuanza vizuri msimu kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii, ambalo kama tutalipata naamini litakuwa sababu kubwa kwetu kuwa na msimu mzuri wa ligi kwa sababu wanasema nyota njema huanza kuonekana asubuhi.

“Naamini kabisa sisi tutashinda mechi hii kwa sababu tumepata muda mzuri wa kujiandaa na kupanga mipango yetu vizuri kabisa, yaani kikosi tulichonacho kinanipa imani kabisa ya kuona tayari tumeshawamaliza Yanga ila kilichobakia ni kwenda kukithibitisha uwanjani tu,”alisema Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI
Read more »


Friday 18 August 2017

TAZAMA Mapokezi ya Majeruhi wa ajali ya basi la Wanafunzi, katika uwanja wa ndege KIA



Watanzania wamejitokeza kuwapokea manusura watatu wa ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha wakitokea Marekani ambako walikuwa wanapatiwa matibabu.

Read more »


Saturday 12 August 2017

HARUNA NIYONZIMA ATEMA CHECHE AWAPIGA YANGA MKWARA MZITO!!!!!


Niyozima Awapa Shule Yanga
KIUNGO mpya wa kimataifa wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amewafichulia wapinzani wao wote wa Ligi Kuu Bara mambo ya ndani kuhusu kiwango chao akiwataka kujipanga vilivyo kuelekea ligi hiyo hapo Agosti 26, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima alisema kiwango walichoonyesha katika mechi dhidi ya Rayon ni sehemu ndogo ya "ufundi" walionao wachezaji wa timu hiyo ambao msimu ujao wamejipanga kuipa klabu yao mataji.

Kiungo huyo aliyetua Simba hivi karibuni kwa kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, alisema kila mchezaji aliyesajiliwa Simba anafahamu kiu ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao wamekosa ubingwa kwa miaka minne.

Niyonzima alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kujifua na kabla ligi haijaanza, watakuwa wameimarika zaidi kwa sababu wachezaji wote wamekamilika na wanafanya mazoezi ya pamoja.

"Tutakuwa wazuri zaidi ligi itakapoanza, tulionyesha kiasi kidogo tu cha uwezo wetu, naamini mashabiki wetu watafurahi zaidi," alisema kiungo huyo wa zamani wa APR.

Naye kipa Aishi Manula alisema kuwa kikosi chao kinaimarika zaidi kila siku zinavyoongezeka huku ushindani wa namba ukiongezeka.

"Kambi ilianza kwa makundi, baadhi tulikuwa katika timu ya Taifa (Taifa Stars) na wengine mchakato wa usajili ulikuwa haujakamilika, sasa tuko pamoja na tunaahidi kuendelea kujituma," alisema kipa huyo aliyetua Msimbazi akitokea Azam FC.

Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema kuwa wako katika mazungumzo ya mwisho ya kupata mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Read more »


Friday 21 July 2017

ERASTO NYONI ATIBUA MIPANGA YA YANGA HATI HATI ZA KUAMSHA DUDE ZA DHIHIRIKA

Image result for ERASTO NYONI


Kuna taarifa kwamba kuwa kusaini kwa kiraka, Erasto Nyoni Simba kumevuruga mipango ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina kwenye kikosi chake.

Kiraka huyo, inaelezwa aliingia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili Simba pamoja na Said Mohamed 'Nduda'.

Awali, kiraka huyo ilielezwa kufikia makubaliano mazuri na Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa kutoka ndani ya Yanga, Kocha Lwandamina ndiye aliyetoa mapendekezo ya usajili wa mchezaji kiraka atakayemudu kucheza nafasi zaidi ya moja kwenye kikosi chake.

Mtoa taarifa huyo alisema walifikia makubaliano mazuri na kiraka huyo kwa asilimia 50, lakini wakashangazwa na taarifa za kusaini Simba mkataba wa miaka miwili.

"Tukiri ni kweli kabisa Nyoni tulikuwa naye kwenye mipango mizuri na mazungumzo yetu yalikuwa mazuri, hivyo tulishangaa kusikia amesaini Simba.

“Kikubwa kocha ndiye alikuwa anaomba asajiliwe mchezaji mmoja kiraka mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja, kwa maana siku akitokea mchezaji mmoja majeruhi au mwenye adhabu ya kadi, basi yeye anaziba nafasi yake,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kauli hiyo ilithibitishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika bila ya kumtaja mchezaji huyo, akisema: “Katika usajili wetu, kuna wachezaji tuliokuwa nao kwenye mipango ya kuwasajili, lakini tumewakosa, hivyo tunatafuta wengine wenye uwezo.”
Read more »


Tuesday 18 July 2017

ESCROW YAIBUKA NA NGELEJA TRA YAMKANA MCHANA KWEUPE WAKKATI MGUMU ZAIDI !!!!!!!!



Waziri wa Nishati na Madini wa zamani Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedha zinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow, lakini akatangaza kuzirejesha kwa TRA Jumatatu iliyopita.

Februari 2014, Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.

Hata hivyo, wakati Ngeleja akithibitisha kwa risiti mbele ya waandishi wa habari kuziingiza fedha hizo katika akaunti ya TRA, mamlaka hiyo imesema haizitambui. TRA imesema haina mpango wowote wa kufuatilia fedha hizo kwa sababu shughuli yake ni kukusanya kodi.

Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.

Kayombo alitoa ufafanuzi huo wakati alipoulizwa na Nipashe juu ya utaratibu rasmi uliopo wa urejeshaji wa fedha hizo endapo wanufaika zaidi wa mgawo wa Rugemalira watataka kufuata nyayo za Ngeleja.

Akifafanua zaidi juu ya suala hilo, Kayombo alisema TRA haihusiki na fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa hazikuwa mali yake.

Aidha, Kayombo alisema TRA haiwezi kuzizungumzia fedha hizo kwa kuwa hazijawahi kuwa mali yake na kuelekeza watafutwe wenye fedha hizo kwa ufafanuzi zaidi.

“Fedha za Escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si zetu?” Alisema Kayombo. “Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama wanataka kurejesha… siyo sisi.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu aliiambia Nipashe wiki iliyopita kuwa uamuzi wa Ngeleja kupeleka fedha za hizo TRA unazua maswali zaidi kwa kuwa alipewa na Rugemarila, na viongozi wa awamu ya nne ya serikali walisema siyo za umma bali mtu binafsi.

Lakini akizungumza jijini Jumatatu iliyopita Ngeleja alisema amerejesha mgawo huo kwa TRA kwa kuwa pamoja na sababu nyingine, ili kujiweka kando na kashfa.

Alisema aliyetoa mgawo huo ameshakamatwa na Takukuru na ana kesi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Huku akionyesha stakabadhi ya malipo ya Benki ya CRDB tawi la Tower, Ngeleja alisema pia “nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa au tuhuma hizo.”

“Nimesononeshwa na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.”

Alisema alipokea mgawo huo Februari 12, 2014 na Januari 15, 2015 alilipa kodi kwa TRA kiasi cha Sh. 13,138,125 ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya msaada huo aliopewa.

Hakusema ni kwa nini ulipita muda mrefu kati ya kupokea na malipo ya kodi.

Baada ya Ngeleja kurejesha fedha hizo palikuwa na wito kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati waliotaka wote waliopata mgawo huo kurejesha fedha hizo kwa TRA kama alivyofanya waziri huyo wa zamani.

MASHTAKA 12
Rugemalira na mwenzake, mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Singh Sethi walisomewa mashtaka 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 3.

Mashtaka hayo ni pamoja na ya kugushi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya dola zaMarekani milioni 22.1 na Sh. bilioni 309.4 kwa serikali.

Novemba 26, 2014, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwasilisha mjini Dodoma ripoti ya uchunguzi wa kashfa Tegeta Escrow ambapo ilisema Sh. bilioni 306 zilichotwa kutoka Benki Kuu kinyume cha sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo wakati huo, Zitto Kabwe alisoma ripoti na kulithibitishia Bunge kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi walihusika katika ufisadi.

Ripoti ya PAC ilianika orodha ya waliopata mgawo huo kuwa mbali na Ngeleja ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge ambao kila mmoja alipata Sh. bilioni 1.6.

Wengine ni ofisa katika Ofisi ya Rais wakati huo, Shabani Ngurumo aliyepewa Sh. milioni 80, Jaji wa Mahakama Kuu, Eudes Ruhangisa alipata Sh. milioni 404.25 na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Dk. Enos Bukuku, aliyepewa Sh. milioni 161.7.

Katika ripoti hiyo Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, Mbunge wa zamani wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko na Jaji wa zamani wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloisius Mujulizi walitajwa kupatiwa Sh. milioni 40.4 kila mmoja.

Wengine ni ofisa wa TRA, Lucy Apollo Sh. milioni 80.8, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko Sh. milioni 40.2, maaskofu Methodius Kilaini Sh. milioni 80.9 na Eusebius Nzingirwa Sh. milioni 40.4, Padri Alphonce Twimannye Sh. milioni 40.4, maofisa wa Rita Placidus Luoga Sh. milioni 121.2 na Theophil Rugozobwa Sh. milioni 323.4.

BAJETI WIZARA
Mgawo waliopata wabunge, maofisa wa serikali na viongozi wa dini kutoka kwa Rugemalira unatosha bajeti ya mwaka mzima ya miradi ya maendeleo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nipashe imegundua.

Katika miaka mitatu iliyopita ya bajeti (2014/15, 2015/16 na 2016/17), wizara hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, ilitengewa bajeti ya Sh. bilioni tatu kila mwaka, ikiongoza wizara zote 18 kwa kuwa na bajeti ndogo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati wizara hiyo ikiambulia Sh. bilioni moja (theluthi ya bajeti yake ya maendeleo) hadi inapofika robo tatu ya mwaka wa bajeti katika miaka hiyo mitatu, imebainika Sh. bilioni 4.77 zinazodaiwa zao la kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizopatiwa waheshimiwa hao zingetosha kugharamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa mwaka mzima na ‘chenji’
ya Sh. bilioni 1.7 ikabaki.

Katika mwaka uliopita wa fedha, kwa mfano, kati ya Sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni Sh. bilioni 1.19 tu (asilimia 40) ndizo zilizokuwa zimetolewa hadi Aprili 30, mwaka huu kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe.

Chanzo: Nipashe
Read more »


Sunday 16 July 2017

SAMATA AZIDI KUNG'ARA ULAYA KAFANYA MAMBO YA AJABU KATIKA MCHEZO WAO WA JANA DHIDI YA AJAX



Mshambuliaji wa KRC Genk, Mtanzania, Mbwana Samatta akiwatoka wachezaji wa Ajax katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu jana Uwanja wa mazoezi wa The Ajax Future timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
Mbwana samatta aonyesha kiwango kizuri zaidi katika mchezo huo hivyo kajiweka katika nafas nzuri
Read more »