Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ndiye mmiliki mpya wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo.
Manji alinunua kampuni hiyo mwishoni mwa mwaka 2014 na kumalizia malipo mwanzonimwaka mwaka 2015 ilipoluwa rasmi ya kwake.
Tigo
iliuzwa kwenye mnada baada ya wamiliki ambao makao makuu yao ni nchini
Sweden kushindwa kumlipa mtumishi wao ambaye alikuwa akiisimamia ambaye
ni raia wa Uingereza.
Baada
ya Mwingereza huyo kufungua kesi, waajili hao walishindwa kumlipa,
hivyo mahakama ikaagiza kufanyika kwa mnada na kampuni nyingine ya nje
ikainunua Tigo kabla ya kumuuzia Manji.
Hata
hivyo, Manji amekuwa katika misukosuko ikiwa ni pamoja na kufunguliwa
kesi ya kutaka mnada urudiwe hali inatakayopelekea yeye kupokonywa
kampuni hiyo.
“Hii ni kesi ya pili katika zile zinazojulikana ndani ya wiki moja. Lakini wiki iliyopita, kulikuwa na kesi mbili.
“Moja
ni ya madawa ya kulevya ambayo wanamtuhumu kuitumia, lakini nyingine ni
kuhusiana na kutaka kurudiwa kwa mnada wa Kampuni ya Tigo ambayo
ameinunua kwa zaidi ya asilimia 90,” kilieleza chanzo hicho cha uhakika.
“Kama
ulikuwa haujui, Tigo ni kampuni ya Manji ambayo aliinunua baada ya
Mwingereza aliyekuwa akiisimamia kuwashitaki waajiri wake wa Sweden
wamlipe alichokuwa akiwadai. Waliposhindwa, mahakama ikapitisha mnada na
kampuni 20 zikajitokeza kununua.
“Kampuni
moja ya nje ilifanikiwa kununua na baadaye Manji akanunua hisa kwa
asilimia 99. Alilipa kila kitu na hana deni, hivyo tangu mwaka 2014,
amekuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano ya Tigo.
“Lakini
kampuni hiyo ya Sweden iliamua kufungua mashtaka Uingereza, ikashindwa.
Ikaja hapa imeshindwa na sasa imeamua kukata rufaa tena.
“Hii
nilitaka nikueleze tu kuwa Manji amekuwa na kesi tatu ndani ya siku
nane zilizopita. Hasa kama kesho atapanda mahakamani ingawa tuna
asilimia kubwa atapandishwa na bado hawajatueleza kosa lipi hasa la
uhamiaji.”
Hata hivyo, chanzo kilieleza huenda likawa kosa la kuwa na pasi mbili za kusafiria.
“Lile
la wafanyakazi, Manji si mmiliki wa kampuni hiyo, labda kama ni lile la
pasi mbili analotuhumiwa pia. Ingawa yeye katueleza ana pasipoti moja
ya Tanzania na hiyo wanayosema si paspoti kama walivyosema, sasa
tunasubiri tuone.”
Hadi
jana usiku, Manji alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Tafa ya
Muhimbili katika majengo ya Taasisi ya Moyo ya Jakata Kikwete.
No comments:
Post a Comment