Tuesday, 14 February 2017

Makonda amkumbusha Spika kuwapima wabunge kilevi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amemkumbusha Spika wa Bunge. Job Ndugai, kuhusu kusudio lake la kuanza kuwapima wabunge kubaini kama wametumia kilevi kabla hawajaiingia kwenye ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Siku chache baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga, kwenye baraza lake la mawaziri kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, Ndugai alisema kuwa kuna wabunge kadhaa huingia bungeni wakiwa wametumia vilevi vikali zaidi vikiwemo bangi, viroba na unga’

Aidha kutokana ba hatua hiyo, Spika huyo alisema wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa kutoa ushauri nasaha wa kisaikolojia, utaratibu huo haujaanza kutolewa bungeni licha ya kwamba ni miezi tisa ipite,

Jana katika hafla maalum ya kukabidhi orodha mpya ya watuhumiwa wa biashara haramu ya madawa ya kulevya Kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzui Dwa za Kulevya, Rogers Siang’a, Makonda alimkumbusha Spika Ndugai kusudio lake la kuanzisha utaratibu wa kuwapima wabunge ulevi.

“Na utaratibu huu wa kuwapima wabunge wetu utakuwa mzuri sana, na ninakumbuka kuna kipindi Spika aliwahi kutangaza kuanzisha lakini sijui ukaishia wapi, nitoe tena rai kwake afikirie tena kuanzisha utaratibu huu ili tuweze kuwabaini wabunge kama wanatumia kilevi ama la,”alisema Makonda.


No comments:

Post a Comment