Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amefunguka kuhusu madai ya
baadhi ya watu kuwa ana utajiri wa kutisha na kwamba anamiliki mali
nyingi, jambo ambalo limekuwa likifanya watu hao watilie shaka njia
aliyotumia kupata utajiri huo.
Kikwete amesema kuwa anashangazwa na dhana hiyo potofu inayojengwa na
watu bila kujua ukweli wa mambo, ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni kijana
mpiganaji na mwenye kupenda mafanikio, lakini hana umiliki wa mali
nyingi kama ambavyo imekuwa ikisemwa.
Ridhiwan ambaye ni mtotot wa Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya
Kikwete, amesema mali zake ni za kawaida na amezipata kwa njia halali,
huku akisimulia jinsi alivyowahi kuwakuta watu wakimjadili yeye kuhusu
mali zake, bila watu hao kujua kuwa yeye ndiye Ridhiwan Kikwete.
No comments:
Post a Comment