Tuesday 28 March 2017

Adhabu waliyopewa Man City baada ya kukiri kushindwa kudhibiti wachezaji wao vs Liverpool


Chama cha soka cha England FA Jumatatu ya March 27 2017 kimetangaza kuipiga faini timu ya Man City kutokana na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji wake wakati wa game ya Man City dhidi ya Liverpool iliyochezwa wiki iliyopita katika uwanja wa Etihad.
Man City ambao walikuwa nyumbani katika uwanja wa Etihad wamekutana na faini ya pound 35000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 98 za kitanzania kutokana na wachezaji wake kumsonga mwamuzi katika mchezo uliyomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.
Tukio la utovu wa nidhamu lilitokea dakika ya 50 baada ya muamuzi Michael Oliver kutoa penati kwa Liverpool, ndio wachezaji wa Man City wakaanza kumzonga muamizi kitendo ambacho kinaashiria kutoridhishwa na kuheshimu maamuzi ya refa katika mechi hiyo iliyochezwa March 19 2017
.


No comments:

Post a Comment