Tuesday 28 March 2017

Nape ampa tano Rais Magufuli na Dkt Mwakyembe kwa uamuzi wa busara dhidi ya Nay wa Mitego


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnaye amempongeza Rais Dkt John Magufuli na Dkt Harrison Mwakyembe kwa busara walioitumia juu ya mwanamziki Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego kuachiwa huru na kuruhusu wimbo wake Wapo uchezwe redioni.
Nape ametongea pongezi hizo Jumatatu hii ikiwa ni ishara ya kupendezwa na uamuzi uliofanyika juu ya Nay wa Mitego.
“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!,” aliandika Nape kupitia akaunti yake ya Twitter.


No comments:

Post a Comment