Warembo wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans
wamedaiwa kuwa wametibuana vibaya kufuatia Chuchu kumchokonoa Johari
mitandaoni kuhusu jina la Kampuni ya RJ, Risasi Jumamosi linakupa ubuyu
kamili.
Chanzo makini kilicho karibu na wawili hao, kimeeleza kuwa, Chuchu
amemchokonoa Johari kwa kutupia picha mtandaoni na kuitangaza muvi
ambayo imezalishwa na Kampuni ya RJ inayomilikiwa na mpenzi wa sasa wa
Chuchu, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wa zamani wa Ray,
Johari kuwa Johari, Chuchu kimenuka tena! imezalishwa na kampuni mpya ya
Ray na mwanaye aliyoiita Rjaden (akimaanisha Ray na mwanaye aliyezaa na
Chuchu aitwaye Jaden).
“Johari alimaindi kweli baada ya kusikia Chuchu amebadilisha jina la
kampuni na kuita kampuni hiyo jina la mtoto wake. Hakupendezwa na hivi
ninavyokwambia wakikutana ni ama za Johari ama za Chuchu. “Johari
ameanza kuona kuna mipango ya kutaka kumuondoa jina lake katika kampuni
na kubadilisha kisanii jambo ambalo hawezi kukubaliana nalo maana si
unajua wamechuma Ray na Johari kwa muda mrefu sana, wamepitia mambo
mengi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Huwezi amini Johari wa watu yupo nyumbani akitafakari cha kufanya maana
anaona kuna mchezo anataka kuchezewa.” Hata hivyo, baada ya Chuchu
kuweka posti hiyo, chanzo hicho kilieleza kuwa alishambuliwa vibaya na
wafuasi wa Johari ambao hawakupendezwa na jambo hilo. “Walimtukana
kweli. Waliona ana mipango mibaya. Si unajua tena mihemko ya mashabiki,
ilikuwa ni kazi kwelikweli,” kilisema chanzo.
Baada ya kutonywa na chanzo ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilimvutia waya
Chuchu na kumuuliza kulikoni hadi awe chanzo cha ugomvi huo kutokana na
kauli yake aliyoandika mitandaoni na kama kweli ana mpango wa kumzunguka
Johari, Chuchu alijibu kwa kifupi na kukata simu. “Hamna kitu kama
hicho,” alisema Chuchu.
Kwa upande wake Johari, alipoulizwa na mwanahabari wetu na kuelezwa kuwa
ameingia kwenye vita mpya na Chuchu ambaye amefuta jina lake katika
utambulisho wa kampuni, Johari alikiri kuiona posti hiyo.
“Nimeiona posti hiyo mtandaoni na nikwambie tu kuhusu la kuchezewa
mchezo, siwezi kukubali kufanyiwa mchezo wowote mbaya… mimi kwa sasa
nipo nyumbani namuuguza mama yangu lakini nikienda ofisini na kukuta
kitu cha tofauti, nitajua cha kufanya,” alisema Johari.
Wawili hao, awali waliwahi kuingia kwenye malumbano kutokana na kitendo
cha Ray kutembea na Chuchu na kumuacha Johari ambaye walitoka naye
mbali. Hata hivyo wawili hao wameendelea kufanya kazi pamoja kupitia
kampuni yao ya RJ ambayo ipo nyumbani anapoishi Ray na mama’ke,
Sinza-Mori jijini Dar.
No comments:
Post a Comment