Friday, 10 March 2017

Kombora No.2 kwa Makonda lampata Mke wake


WAKATI nchi ikiwa imelipuka na kumpigia kelele za kutaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aoneshe cheti halisi cha kidato cha nne na kama hana ajiuzulu, wapinzani wake hao wameibuka na kombora namba mbili ambalo ni uraia wa mkewe, Ijumaa linakudadavulia. Awali, hoja ya vyeti feki ilishikiwa bango zaidi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima ambaye alisema ana ushahidi wa cheti halisi cha Makonda chenye matokeo ya Divisheni 0 na kwamba alitumia cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge kilichomwezesha kuendelea na msomo.
NI JUMAPILI ILIYOPITA Gwajima alitoa madai hayo mazito, Jumapili ya Februari 26, mwaka huu, kwenye mahubiri ya ibada ya kanisani kwake, Ubungo ambapo alisema kuwa, Makonda alitumia cheti hicho feki wakati yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert Bashite.
MITANDAONI SASA Baada ya Gwajima kufunguka hayo, mitandao ya kijamii ilianza ‘kumpiga’ Makonda kwa kumsema vibaya huku baadhi Chunguni
WAZIDI KUMUANDAMA 
Kuna wengine walienda mbali zaidi, baada ya mkuu huyo wa mkoa kwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kimara jijini Dar Jumapili iliyopita na kuangua kilio alipokuwa ibadani, wakasema ‘hata akilia wao wanataka vyeti.’
“Hatutakiwi ulie, toa vyeti baba,” alichangia mmoja wa wafusi wa Mtandao wa Facebook. KUSUDI LA MAKONDA Kwenye ibada hiyo, Makonda alipopewa nafasi ya kuzungumza, alitumia mwanya huo kueleza namna ambavyo ameingia kwenye vita kubwa ya madawa ya kulevya ambayo wengi waliowahi kuianzisha walipoteza maisha ama walifungwa.
Alisema, inahitaji usimame na Mungu wa kweli ili uweze kufanikiwa kuishinda vita ya madawa ya kulevya kwani wanaohusika, wana nguvu kubwa ya kufanya lolote lakini yeye amejitoa mhanga kumsaidia Rais Magufuli aliyemteua.
“Kwenye hii vita, kila aliyeingia ni ama aliuawa au alifungwa au alipotezwa kwa namna yoyote ile,” alisikika Makonda akisema. Kuonesha kwamba yupo tayari kwa lolote, Makonda alisema yeye haoni tatizo kuukosa wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa siku moja lakini hawezi kukubali katika utawala wake, vizazi viangamie kwa madawa ya kulevya.
“Hata kama nitakuwa mkuu wa mkoa kwa siku moja lakini ilimradi nimetimiza kusudi la Mungu, nipo tayari,” alisema Makonda.
ALIGUSIA KOMBORA NO. 2 Katika mazungumzo yake kanisani hapo, Makonda alionesha kunusa harufu ya kombora la pili ambalo ameandaliwa ili kukwamisha jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya ukiacha lile namba moja la vyeti ambalo ndilo lilikuwa ‘hot’.
“Baba mchungaji huwezi amini sasa hivi wametoka kwenye suala la vyeti, wamehamia kwa mke wangu. Naye wanasema si raia,” alisema Makonda.
MITANDAO YAKAZIA SASA Baada ya Makonda kusikika hivyo, mitandao ilizidi kuchochea moto suala hilo na kusema kwamba ni kweli mkewe si raia kwani hata uso wake unaonesha.
“Wewe humuoni alivyo? Anaonekana kama raia wa kigeni hivi, wakimfuatilia watajua na ninaamini ushahidi ni rahisi sana kupatikana. Vimepatikana vyeti sembuse uraia, tutashuhudia mengi mwaka huu,” alichangia jamaa aliyejiita Mehans mtandaoni.
MAKONDA AKESHA AKIMUOMBA MUNGU
Taarifa za ndani zimedai kuwa kutokana na makombora hayo, Makonda ameamua kumshtakia Mungu na kumuacha ayashughulikie maana anaamini dhamira yake ilikuwa njema katika mkoa na taifa lake. “Makonda sasa anapambana kiimani, ameamua akeshe kwenye maombi. Anafanya maombi, anaamini mwisho wa siku Mungu wake atamtetea. Mungu hawezi kukubali aangamie.
Wanamsakama kwa maneno, wanasahau ni Makonda huyo aliyejitoa kinaga ubaga kudhibiti mashoga. “Makonda huyohuyo alijitoa kudhibiti matumizi ya shisha, alisimama kidete kuendesha zoezi la kusalimisha silaha ambalo lilichangia kupunguza uhalifu ndani ya jiji.
“Watu wanajiweka pembeni na hoja ya msingi ya madawa ya kulevya ambayo mheshimiwa amejitoa. Amethubutu kuwataja wahalifu wa madawa hayo  yanayowaangamiza vijana, wao wanang’ang’ania suala la vyeti na uraia wa mkewe kweli? Mungu atampigania,” kilisema chanzo kilicho karibu na Makonda.
MADAI MENGINE
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambazo hazijathibitishwa, zinadai kuwa, kuna uwezekano mkuu huyo wa mkoa akawa amemuandikia barua rais kuomba kujiuzulu ili kuondokana na ‘presha’ ya maadui wanaomsakama. Hata hivyo, Makonda na ofisi ya rais, hawajazungumzia lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoenea.


No comments:

Post a Comment