Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amefanya mkutano wa hadhara ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipotoka mahabusu wiki moja iliyopita.
Lema amefanya mkutano huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro ili kuweza kuzungumza na wapiga kura wake kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya maendeleo katika jimbo hilo.
Miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, Godbless Lema amezungumzia kukamatwa kwake ambapo amesema kuwa amekaa mahabusu kwa miezi minne pasipo kuwa na kosa kabisa.
Aidha, ameeleza kuwa mahabusu kuwa watu wengi ambao wapo kule kwa kusingiziwa wengine wamewekwa tu kwa uonevu na hawana kosa, hivyo kama kiongozi ataendelea kuwapigania huku akiwasihi wakazi wa Arusha kuwaombea waliopo mahabusu.
Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza leo ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama mkoani humo akiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro.
No comments:
Post a Comment