Jopo la Makardinali waliompa ushirikiano mkubwa Papa Francis wa 16
wakati wa uteuzi wake, wamepanga kumshinikiza ajiuzulu kutokana na
ukiukwaji wa maadili ya kanisa.
Gazeti la The Times na Libero la Italia, yameandika kuwa Makardinali hao
zaidi ya dazeni, wamepanga kushinikiza Papa Francis ajiuzulu lakini
bila kujitenga naye kwa namna yoyote ile. Hata hivyo haijafafanuliwa ni
maadili gani aliyoyavunja Papa huyo.
Makardinali hao ndiyo waliofanya jitihada kubwa za kuteuliwa kwa Papa Francis katika uteuzi wa nafasi hiyo mwaka 2013.
Mwandishi Antonio Socci ameandika katika gazeti la Libero na kueleza
kuwa kwa sasa Makardinali wanajadili iwapo Papa akijiuzulu nani
atashika nafasi yake.
No comments:
Post a Comment