Saturday, 25 March 2017

Mamilioni ya wafanyakazi duniani hatarini kupoteza kazi

Leo March 25, 2017  imeripotiwa taarifa ya utafiti inayodai kuwa kuwa mamilioni ya wafanyakazi duniani wapo hatarini kupoteza kazi zao kutokana na matumizi ya Sayansi na Teknolojia.
Katika utafiti huo mpya uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa kazi nyingi zitakuwa zinafanywa na robots miaka 15 ijayo ambapo Marekani ikiongoza kwa 38% ya kazi nchini humo zitafanywa na robots, kwa mujibu wa utafiti mpya wa PwC.
Wakati huo huo, 30% ya kazi Uingereza zitafanywa na robots, Ujerumani ni 35% huku Japan ikiwa 21% ya kazi ambazo zitafanywa na robots katika miaka 2030.
PwC imezitaja pia sekta zitakazoondoa watu wengi zaidi kwenye kazi na kutumia robots kuwa ni Usafirishaji, Viwanda, Maduka makubwa ya Jumla na Rejareja na sehemu ndogo katika Elimu, Afya na kazi za jamii. Wafanyakazi wa kiume wametajwa kuwa hatarini zaidi kupoteza kazi kuliko wanawake.


No comments:

Post a Comment