Asalaam Allleikhum wana Dar es salaam. Baada ya Salamu, naomba nitoe
shukrani kwake Mwenyezi Mungu wa mbingu na ardhi, anayetupa pumzi ya
kuhema bila malipo, yeye atoae uzima kwa vinavyo onekana na visivyo
onekana, sifa na utukufu virudi kwake maana hakuna kama yeye.
Leo ninarudi ubaoni nikiwa na majibu kwa Wananchi wote waliopo Dar es
salaam na nje ya Dar es salaam mliopata kunipigia na kunitumia sms juu
ya *"KASHFA YA KUGUSHI VYEKI"* Inayo mkabili moja wa viongozi wa Mkoa wa
Dar es salaam.
Mosi, Mimi kama nguzo na Kiongozi mmoja wapo ninae unda uongozi wa
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ninajibu kwa niaba yangu au kwa
ukaribu wa mashirikiano baina ya serikali kuu na serikali za mitaa Dar
es salaam, kwa maana zipo namna nyingi tunahitaji kushirikiana na
uongozi wa serikali kuu Dar es salaam, kwa hiyo lolote kuhusu Dar es
salaam yanatuhusu sote ndiyo maana hatuwezi nyamaza.
Pili, ya kwamba Ofisi ya Mkoa Dar es salaam, ikikumbwa na kadhia na
kashfa kubwa kiasi hiki kwa namna yeyote sisi wawakilishi pekee wenye
dhamana Dar es salaam kwakuwa sisi ndiyo tumechaguliwa wengi kuongoza
Dar es salaam, kwa madiwani wengi, wabunge wengi; kwa hiyo basi
ukinajisi ofisi ya mkoa kwa kuwa na kashfa ya "UHALIFU WA KITAALUMA"
basi ni sisi viongozi wa kuchaguliwa na wananchi tunapaswa kutoka na
kuwasemea Wakazi wa Dar es salaam kwakuwa dhamana hiyo tunayo sisi.
Sisi Viongozi wenu tupo imara na tuna wahakikishia kuwa DAR ES SALAAM,
haita kaa kamwe iongozwe na "KILAZA" na si tu KILAZA bali "MUHALIFU WA
TAALUMA". Njia pekee ya Mameya, wabunge ma Madiwani Dar es salaam kutoa
ushirikiano na serikali kuu ni moja kati ya haya yafanyike.
1. Utolewe ufafanuzi juu ya kashfa hiyo kwa kiongozi muhusika kujitokeza na vyeti vyake vyote na kuvianika hadharani.
2. Serikali imsafishe haharani kama wanayo taarifa nyingine zaidi ya
hizi walizonazo wananchi, au serikali imchukulie hatua kama muhalifu
mwingine yoyote bila kujali cheo chake, chama chake au ukaribu na mkuu
wa nchi.
Vinginevyo sisi kama viongozi wa Dar es salaam tumefedheheshwa sana
Kusikia kashfa hiyo ya kugushi vyeti kwa kiongozi wa Mkoa wa Dar es
salaam, na bila ya unafiki inatuwia ngumu kufanya naye kazi yoyote bila
ya kupata ufafanuzi binafsi wa muhusika kwakuwa viongozi wenzie
Tumeathiliwa kisaikolojia......hivyo kila anachokifanya tunakihusisha na
kufeli kwake na kugushi kwake vyeti vyake vya taaluma.
Kwa mfano .....
1. Tangu Mwaka jana mwezi march ajawahi kuitisha kikao cha mashauriano
cha mkoa wa Dar es salaam; na ikumbukwe vikao vya mashauriano mkoani ni
vya kisheria na yeye ni mwenyekiti wa vikao hivyo, kwa mwaka vinapaswa
kukaliwa mara nne. Je tunajiluza kama kazi yake namba 1 anashindwa
kuifanya anajua kweli wajibu wake? Na kama hajui, je ni kufeli na
kugushi kwake ndio kumepelekea kushindwa kumudu majukumu yake hayo?
2. Tangu mwaka jana mwezi march hajawahi kuitisha kikao cha bodi ya
narabara na ilhali yeye ni mwenyekiti. Wabunge na Mameya ni wajumbe, hii
ni kazi yake muhimu katika kazi zake kuu tatu, je alikuwa hajui wajibu
wake au ni kufeli na kugushi kumepelekea kushindwa kumudu majukumu yake?
3. Waziri mkuu yupo mkutanoni anaongelea Maswala ya umeme, waliopo mbele
na wafanyakazi wa TANESCO,wewe unaongelea SHISHA, kama si UBASHITE ni
nini?
Mwanzo wakati anafanya hivyo tuliona kawaida ila baada ya haya yote
tunajiuliza huenda kufeli kwake na kugushi vyeti kulisababishia yote
haya.
Na mengine mengi tu, ambayo kimsingi sisi kama viongozi wa UKAWA Dar es
salaam , Mameya, Wabunge na Madiwani tunasitisha mashirikiano na ofisi
ya mkuu wa mkoa mpaka pale tutakapo pata usahihi wa kashfa hii kwenye
ofisi ya mkoa, ili tusiendelee kuathirika kisaikolojia ni vyema kiongozi
binafsi au serikali itufumbulie fumbo hili, ambapo tangu serikali ya
awamu ya tano iingie madarakani, haijawahi kuwa na kigugumizi isipokuwa
kwenye jambo hili.. kunaniii?
Wenu katika ujenzi wa Taifa
BONIFACE JACOB(Senior councilor),
KATIBU WA MAMEYA CHADEMA TANZANIA,
MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA,
MSTAHIKI MEYA UBUNGO.
No comments:
Post a Comment