Wednesday, 1 March 2017

POGMA AWEKA REKODI NYINGINE MPYA UINGEREZA....................

Kadri siku zinavyokwenda ndiyo jinsi Manchester United wanavyoonekana bora.Na kadri United wanavyozidi kuwa bora ndio Paul Pogba anavyozidi kuwa bora.Ubora wa eneo la kiungo cha Manchester United umeimarishwa sana na Pogba huku uwepo wa Ander Herrera na Michael Carrick vikizidi kumfanya awe bora.
Aina ya uchezaji wa Pogba unawapa United faida kubwa sana.Pogba sio aina ya kiungo anayekaa sehemu moja kufanya kazi moja,Pogba anakuwa huru sana uwanjani akionekana kurudi nyuma kukaba,anavyochukua mipira kuipeleka mbele.Lakini Pogba pia anaisaidia United katika kishambulia na ndio maana sio jambo la ajabu yeye kuwepo kwenye orodha ya wachezaji waliogongesha mwamba mara nyingi.
Sasa Pogba ameweka rekodi nyingine mpya Uingereza.Pogba anakuwa mchezaji wa kwanza katika ligi ya Uingereza msimu huu kupiga pasi 1000 katika nusu ya eneo la wapinzani.Hii inaonesha jinsi gani kiungo huyu alivyo msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Manchester United katika msimu huu wa ligi.Pengine hili pia linawafanya United wasijutie kiasi kikubwa cha pesa walichotoa kumnunua Paul Pogba.
Jambo la kuvutia zaidi kwa Pogba ni kwamba anaweka rekodi hii huku wanaomfuata wakiwa wamecheza mechi nyingi kuliko yeye.Jumla ya pasi hizi alizopiga Pogba ni 1029.Katika orodha hii,viungo 10 wanaoongoza kupiga pasi hizi yupo mchezaji mwingine wa Manchester United Ander Herrera ambaye yuko nafasi ya 6 akiwa amepiga pasi 827.Hii inaonesha muunganiko wa Pogba na Herrera umeleta nguvu mpya Man United katika sehemu yao ya kiungo.
Wakati Pogba anaongoza kwa pasi nyingi kwenye nusu ya wapinzani,anayemfuatia ni Jordan Henderson wa Liverpool mwenye pasi 987.Mesut Ozil wa Arsenal yuko nafasi ya tatu akipiga pasi 957,David Silva wa Man City yuko nafasi ya nne akiwa amepiga pasi 930 na Eden Hazard nafasi ya tano akiwa na pasi 875.


No comments:

Post a Comment