Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango vya soka vinavyotolewa
na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kutoka nafasi ya 158 mwezi Februari
hadi nafasi ya 157 mwezi Machi, kati ya wanachama 211 wa FIFA
Kwa mujibu wa viwango hivyo vilivyotolewa , Argentina imeendelea kubaki
katika nafasi yake ya kwanza ikifuatiwa na Brazil, huku Ujerumani
ikibaki nafasi ya tatu ikifuatiwa na Chile, Ubelgiji, Ufaransa,
Colombia, Ureno, Uruguay, na Hispania ikiwa katika nafasi ya 10
Bara la Afrika linaongozwa na Misri ikiwa imepanda nafasi 3 hadi nafasi
ya 20, ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 28 na mabingwa wa Afrika
Cameroon wanafuata wakiwa nafasi ya 32 ambapo wamepanda kwa nafasi moja.
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda inakamata nafasi ya 74
ikiwa imekwea kwa nafasi moja, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 88, Rwanda
nafasi ya 93, Ethiopia nafasi ya 104, Sudan 138, Tanzania 157 huku
Somalia, Djibout na Eritrea zote zikiwa mkiani katika nafasi ya 205.
No comments:
Post a Comment