Tuesday 14 March 2017

TOP 10: Wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi kwa haraka zaidi duniani

 
Mchezo wa soka ni miongoni mwa michezo inayopendwa zaidi duniani huku wachezaji wakivuna kipato kikubwa kutokana na uhodari wao kuhakikisha wanatumikia klabu zao vizuri.
Nahodha wa Ureno na nyota wa club ya Real Madrid Cristian Ronaldo ametajwa kuwa ndiye mwanamichezo anayeingiza kipato kikubwa kwa haraka zaidi duniani akimzidi mpinzani wake katika soka Lionel Messi wa FC Barcelona.
Katika utafiti uliotolewa na Expert Market UK Cristiano Ronaldo anahitaji saa 45 au jumla ya siku za kazi 5.68 kuvuna pound milioni moja huku Lionel Messi akihitaji siku 5.96 kuingiza kiasi hicho.
Expert Market UK inawataja pia katika list hiyo madereva wa Formula One Lewis Hamilton na Sebastian Vettelnyota wa American football Eli Manning na boxer Floyd ‘Money’ Mayweather.
Wengine ni nyota wa baseball Ryan Howard na nyota wa Real Madrid Gareth Bale anayetimiza idadi ya wachezaji wa soka watatu kwenye Top 10.
Nimekusogezea hapa list ya wanamichezo 10 wanaoingiza fedha nyingi kwa muda mfupi
NafasiJinaMchezoMuda/siku za kuingiza paundi 1 million
1Cristiano RonaldoFootball5.68
2Lionel MessiFootball5.96
3Joe FlaccoAmerican football7.23
4Lewis HamiltonFormula 17.57
5Sebastian VettelFormula 17.96
6Eli ManningAmerican football8.60
7Floyd MayweatherBoxing9.93
8Ryan HowardBaseball12.72
9Gareth BaleFootball12.77
10Lebron JamesBasketball13.71


No comments:

Post a Comment