Thursday 9 March 2017

Video: Rais Magufuli aipai shavu Muziki ya Darassa mkutanoni



Nadhani Darassa sasa ana kila sababu ya kuachia ngoma mpya baada ya wimbo wake, Muziki kupata endorsement toka kwa kila mtu, hadi kutoka kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli

Dkt Magufuli ambaye yupo ziarani kwenye mikoa ya Kusini, alijikuta akiinukuu mistari kadhaa ya wimbo maarufu wakati akizungumza na wananchi.
“Kwamba unaenda bila break, what do you expect,” alisema Rais Magufuli na kuchochea shangwe la haja toka kwa wananchi wanaojua wimbo huo kabla ya kuongeza, “Mkishaimbiwa changanya kama karanga ndio mnachanganyikiwa kabisa.”
Darassa hajachukulia poa shavu hilo. Ameandika kwenye Instagram: THANK YOU PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.”
Kazi kwako Darassa!


No comments:

Post a Comment