Tuesday 18 April 2017

SAMATTA AZIDI KUNG'ARA SASA ASAKWA NA KLABU ANAECHEZEA VAN PERSIE KWA DAU NONO


Fenerbehce ya Uturuki imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambulizi Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji ambako amekuwa aking'ara.

Kwa sasa, mkongwe Robon van Persie ndiye kiongozi wa ushambulizi katika timu hiyo ya pili kwa ukubwa nchini Uturuki baada ya Galatasaray.

Lakini  Fenerbehce  inaonekana imeamua kujiimarisha na sasa inasaka mshambulizi kijana na hatari, Samatta anatupiwa jicho.


Wengine ambao wanapewa nafasi ya kusajiliwa na Fenerbehce  ni Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps.


No comments:

Post a Comment