WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema itawachukulia hatua watu wote walioshindwa kutimiza wajibu wao katika ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vincent ya Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na kila atakayebainika hakutimiza wajibu wake atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
Mei 6, mwaka huu, kulitokea ajali kwenye mlima wa Rhotia wakati wanafunzi hao walipokwenda kufanya mitihani ya ujirani mwema katika Shule ya Tumaini Junior iliyopo Wilayani Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32.
No comments:
Post a Comment