Friday 19 May 2017

VIDEO-TAZAMA KIKAO KILICHO FANYIKA NDANI YA SHULE YA LACK VICENT NA KUSABABISHA VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI KUKAMATWA NA POLISI

Image result for MKUTANO ULIOFANYIKA JANA KATIKA SHULE YA LUCKY VINCENT
Jana May 18 kwenye shule ya Lucky Vicent Arusha, Polisi walivamia mkutano ulioongozwa na Meya wa jiji hilo akiambatana na viongozi wa dini, Madiwani na Waandishi wa habari ambao Meya alidai lengo lake ni kukabidhi rambirambi walizozichanga wao kutokana na msiba wa ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Wakati viongozi hao wakiendelea kuhojiwa na Polisi Arusha, millardayo.com na AyoTVzinakukutanisha na video ya sehemu ya vilivyokua vinazungumzwa ndani ya mkutano huo kabla ya Polisi kuvamia.

Hii video hapa chini Katibu wa chama cha Wamiliki wa Shule binafsi mkoa wa Arusha Leonard Mao alikua anaongea

“Nilitangaza kwa niaba ya Watanzania siku ya kuaga ile miili 35 kwamba tutaendelea kuchanga rambirambi zetu na kwenda kuwaona wale wazazi mmoja baada ya mwingine“

“Hakuna hata senti ya mtu itakwenda pembeni…. hatumpi mtu hata kwenye shule ya Vicent, ni waliofiwa wenyewe mkono kwa mkono

’ FULL VIDEO NDIO HII HAPA CHINI UNAWEZA KUPLAY UKAJIONEZA ZAIDI: 



My take, ni uhuni uliopindukia kuvamia na kuharibu shughuli ya uwasilishwaji wa rambirambi zilitolewa kwa wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki laana iwe juu ya yeyote aliyehusika na uhuni huu.


No comments:

Post a Comment