Leo mchana kwenye majira ya saa tisa, msanii Rayvanny aliwasili nchini akiwa na tuzo yake ya BET ambayo aliinyakuwa usiku wa Jumamosi nchini Marekani aliwasili katika uwanja wa JK. Nyerere na kupata mapokezi makubwa kama ya kifalme.

Msanii huyo aliongozwa na msafara mkubwa pamoja na mashabiki wake na kuanza kuitembeza tuzo hiyo katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Buguruni, Kariakoo, Magomeni, Tandale, Sinza na Mikocheni.













No comments:
Post a Comment