Wednesday 15 February 2017

Ancelotti: Na muheshimu sana Arsene Wenger anafaa kupongezwa




Kocha wa klabu ya Bayern Munich Carlo Ancelotti amesema kuwa anamuheshimu sana kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na kusema kuwa kocha huyo ataweza kujinasua kutoka kwa shutma ambazo zimekuwa zikimkabili hivi karibuni.

Matokeo mabaya katika ligi ya Uingereza yameongeza uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ufaransa huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakimtaka aondoke.
Ancelotti anaamini kwamba Wenger anafaa kupongezwa kwa kazi aliyofanya.
”Alijenga kitambulisho na mbinu nzuri ya kusakata soka” ,alisema raia huyo wa Itali.
”Wenger ana uzoefu wa kujua kwamba katika kazi yetu ni swala la kawaida kukosolewa.
kwa hilo hana tatizo. Ninaheshimu sana kazi aliyofanya katika klabu ya Arsena”
Ancelotti ambaye aliwahi kuwa kocha wa Chelsea alikuwa akizungumza na waandishi kabla ya mechi ya leo Jumatano ya klabu bingwa ya Ulaya awamu ya kwanza kati ya timu hizo mbili nchini Ujerumani.


No comments:

Post a Comment