Manji na Wafanyakazi Wake 25 Kupanda Kizimbani Leo...!!!!
Wafanyakazi 25 wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na
mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, wanaodaiwa kutokuwa na
vibali vya kufanya kazi nchini, leo wataanza kujieleza kwa maandishi
katika ofisi za uhamiaji.
Ofisa uhamiaji wa mkoa, John Msumule amesema uhamiaji haijawakamata
wafanyakazi hao, isipokuwa inashikilia hati zao za kusafiria.
“Kesho (leo) tunatarajia kuanza kuwahoji ili watoe maelezo yao, ikiwa ni
hatua ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani Jumatatu ili kuwezesha
hatua nyingine za kisheria kuchukua nafasi yake.”
Mbali na wafanyakazi hao, Manji anasubiriwa na sekeseke jingine la
uhamiaji baada ya kuitwa ili aunganishwe na wafanyakazi hao kushtakiwa
kwa madai ya kuajiri wageni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.
Manji amekuwa akishikiliwa na polisi tangu Februari 9 alipoitikia wito
wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kuripoti kituo kikuu cha polisi kwa
ajili ya mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Ofisa uhusiano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Anna Nkinda
amesema Manji aliruhusiwa hospitali jana saa 10:00 jioni baada ya
kupatiwa matibabu kwa siku tatu. Hata hivyo haikufahamika alikokwenda.
No comments:
Post a Comment