Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza
la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo
huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo
huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa
ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na
hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram.
“Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila
kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za
BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote
pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na
siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari
ili usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio
wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU
n.k.”
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook: Serikali
imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni
utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”
No comments:
Post a Comment