Naibu
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha
na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia
mitandao ya kijamii.
Naibu
Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo
alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea
jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo
hadharani.
Aidha,
amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali
itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.
Kigwangalla
ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si
suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo
watakahikikisha wanalikomesha.
No comments:
Post a Comment