Thursday, 2 March 2017

Maoni ya Zitto Kabwe Kuhusu Uteuzi wa Mama Salma Kikwete na Kuhusu Baa la Njaa


Serikali Ina Kauli Mbili Zinazokingana Juu ya Hali ya Chakula Nchini

Siku nzima ya jaa nilikuwa natakiwa na waandishi wa Habari kutoa maoni yangu kuhusu uteuzi wa Mtanzania mwenzetu, na mke wa Rais aliyepita, Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Niliwaambia sina maoni yeyote. Leo baada ya magazeti kuandika maoni ya watu mbali mbali nimeulizwa tena. Jibu langu, ambalo ninaliweka hapa kwa umma, ni kwamba Mama Salma Kikwete ana haki zote kama Mtanzania mwengine yeyote kuteuliwa ama kuchaguliwa Kwa mujibu wa Katiba yetu. Hivyo uteuzi wake kwa maoni yangu ni kama teuzi nyengine zozote zile.
Kuolewa kwake na aliyekuwa Rais hakumwondolei yeye haki zake za kikatiba. Kama mwenyewe ataridhia ninamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya. Sababu za kuteuliwa kwake anajizuia aliyemteua na baadhi ya wasomi wabobezi Kama Prof. Kitila Mkumbo wamenukuliwa wakifanya uchambuzi mzuri Kabisa kwenye gazeti la The Citizen la Leo.
Kwangu Mimi, kwa maoni yangu, nchi yetu inakabiliwa na mambo makubwa zaidi ya kujadili na kutolea maoni ikiwemo suala la njaa. Serikali kwenye suala hili la njaa imeyumba sana na kwa kiasi flani imewayumbisha pia wananchi wanyonge wanaokabiliwa na tatizo hili, na kwa maoni yangu naamini kabisa Serikali haijatekeleza wajibu inavyostahili. Kama mzalendo kwa taifa langu nachukua wajibu wangu kuonyesha mapungufu hayo ya Serikali pamoja na kutoa njia mbadala.

Jana, Serikali kupitia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa haitatoa chakula cha msaada kwa Watanzania watakaokabiliwa na njaa. Rais alisema "tumezoea kuambiwa maneno matamu matamu kwamba hakuna mtu atakeyekufa kwa njaa. Mimi nawaambia usipolima utakufa na njaa". Serikali kwa kauli za namna hii inawachanganya watanzania, kwanza ni muhimu sana kujua (na naamini Serikali inajua) kuwa wananchi hawa wamelima, suala la hali ya njaa si kwa sababu ya kutokulima kwao, bali ni kwa sababu kadhaa zilizo nje ya uwezo wao, ikiwemo hali ya hewa yenye mvua chache.
Mfano mikoa ya Singida, Shinyanga


No comments:

Post a Comment