Mambo yanayomtokea kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ni kama mchezo wa kuigiza.
Jana, Lissu alianza siku kwa furaha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa
Kisutu kumuona hana kesi ya kujibu, lakini dakika chache baadaye polisi
walimkamata tena, kumhoji na kumuachia kwa dhamana.
Licha ya kashikashi hizo mahakamani na kituo cha polisi, Lissu
ameonyesha kuwa na sakata jingine katika uchaguzi wa Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika (TLS) baada ya kudai kuwa kuna mkakati unasukwa
na baadhi ya mawakili wenzake kutaka kumkwamisha asigombee urais wa
chama hicho.
Baada ya kuachiwa huru, Lissu alikamatwa na polisi akiwa Mahakama ya
Kisutu na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi, lakini haikueleweka sababu
za kukamatwa kwake.
Lissu alikutana na polisi hao saa 4:00 asubuhi na akaambiwa kuwa
anahitajika kituoni, mbunge huyo aliomba aendeshe gari lake mwenyewe
ambalo alikuwa nalo Kisutu.
Wakili wake, Fredrick Kihwelo alisema: “Polisi walikubaliana naye na
kuingia kwenye gari lake na kuelekea kituoni hapo na walipofika walikaa
muda kisha wakaelezwa kuwa, anadaiwa kutoa
matamshi yanayoweza kusababisha matatizo ya kidini.”
Alisema Lissu alidaiwa kutoa matamshi hayo akiwa mkoani Dodoma, hivyo
baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni
hapo Machi 13.
No comments:
Post a Comment