Friday 21 April 2017

DAH! BASI NDIYO HIVYO, YAANI KIDOGO TU SAMATTA AMEIKOSA MAN UNITED




Mshambuliaji Mbwana Samatta, ameikosa kidogo tu Manchester United, jambo ambalo Watanzania wengi wapenda soka walitamani litokee.


Kikosi cha KRC Genk anayoichezea Samatta imeng’olewa kwenye michuanon ya Europa Cup hatua ya robo fainali, kwa kufungwa jumla ya mabao 4-2 na Celta Vigo ya Hispania.


Sasa Vigo ndiyo wamepangwa kukutana na Man United katika hatua ya nusu fainali na kama Genk wangevuka, maana yake wangekutana.



Genk ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya nyumbani baada ya Celta Vigo kuwa imeshinda awali kwa mabao 3-2.


No comments:

Post a Comment