Tuesday 2 May 2017

BIASHARA YA KUBET YAMWINGIZA MKENYA KATIKA REKODI YA DUNIA YAMKUTANISHA NA STAA HUYU


Biashara ya kubet imekuwa ikishika kasi barani Afrika kila siku huku makampuni mengi yakianzishwa na kujikusanyia watu wanaopenda kufanya hivyo.
Leo May 2, 2017 good news kwa watu wangu wanaopenda michezo ya kubahatisha ‘betting’ kwamba wasikate tamaa kwa sababu upo uwezekano mkubwa wa kushinda kama ambavyo Mkenya huyu ameshinda.
Mtandao maarufu wa BBC umeripoti kuwa Samuel Abisai, 28, kutoka Kenya ameshinda Dollar 2m (£1.6m) zaidi ya Tsh. 4.5b baada ya kushinda utabiri wa mechi 17 za kandanda na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kushinda kiasi hicho cha fedha kupitia betting kwenye historia ya soka la Afrika.
Samuel ameshinda kiasi hiko cha fedha baada ya kutumia Dollar 2 kwa machaguo mawili tofauti, kwa mujibu wa SportPesa ambapo kutokana na ushindi wa fedha hizo, Abisai anapanga kutoa sehemu ya ushindi huo kwa jamii yake, ikiwa ni pamoja na kuisaidia klabu yake ya mtaani mkoa wa Magharibi wa Kakamega.
VIDEO: Binadamu mzee zaidi duniani anayepatikana Tanzania. Bonyeza play 


No comments:

Post a Comment