Tuesday, 2 May 2017

SAKATA LA WENYE VYETI FEKI LIMEWASHANGAZA WENGI BAADA YA KUMUANGUKIA MWENYEKITI WA CCM



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Chamwino, Charles Ulanga ameshangazwa baada ya kutajwa miongoni mwa watu wenye vyeti feki cha kidato cha nne na kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya sekondari.

Sakata la Mwenyekiti huyo ni mwendelezo wa utata ulioibuka baada ya ripoti ya matokeo ya uhakiki huo uliobaini wafanyakazi 9,932 wa Serikali na Taasisi zake kuwa na vyeti vya kughushi, kutumia vya watu wengine au cheti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja.

Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, amesema wakati wa uhakiki alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu ‘A’.

“Nawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?” amehoji Ulanga.


No comments:

Post a Comment