Tuesday 2 May 2017

Himid Mao afata nyayo za Samatta akwea pipa kwenda Denmark kwa majaribio ya Randers FC


Mchezaji wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars, Kiungo Himid Mao amekwea pipa jana jioni akielekea nchini Denmark, kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa katika bara la Ulaya.
Kiungo huyo machachari anakwenda kufanya majaribio yake ya soka la kulipwa katika klabu ya Randers FC ambayo iko katika ligi kuu nchini Denmark maarufu kwa jina la Superliga.
Mao amekuwa katika kiwango cha juu katika ligi ya msimu huu pamoja na michuano mingine ambayo kiungo huyo amekua akicheza.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo akisema, “Tuna wachezaji zaidi ya sita wameenda ulaya kwa majaribio, na Mao ni mmoja wao. Taarifa zingine tutatoa kama klabu ila Mao ana baraka zote za klabu kuondoka. Amepata nafasi ya kuondoka, na hakuna atakaemzuia, wote wataondoka na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wote tunaamini watafanikiwa na wataweza kuanza maisha mapya katika nchi moja wapo,”


No comments:

Post a Comment