Wednesday 17 May 2017

KUFUATIA VIONGOZI KADHAA KUACHIA NGAZI KATIKA SERIKALI YA JPM,HUU HAPA NI UTEUZI MPYA ULIOFANYA NA RAISI LEO!!!!!!!!

Image result for MAGUFULI

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo (Jumatano) amemteua Geoffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya uteuzi huo Mwambe alikuwa mkuu wa wilaya ya Manyoni. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.

Tandari anachukua nafasi ya Dk  John Ndunguru ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo  Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Uteuzi huo unaanza mara moja.


No comments:

Post a Comment