Monday, 1 May 2017

WEMBE ULIOWAKATA WENYE VYETI FEKI SASA WAANGUKIA WATUMISHI WA UMA RAISI AJA NA KAULI HII .....



RAIS Dk. John Magufuli amesema serikali itawachuguza na kuwachukulia hatua baadhi ya wafanyakazi ambao wamebadili umri wao ili waendelee kuwepo kwenye ajira serikalini.

Akizungumza jana kwenye sherehe ya sikukuu ya wafanyakazi dunia zilizofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanajaro, alisema wapo wafanyakazi ambao wamebadilisha umri wao na wanaendelea kuwepo kwenye ajira licha ya kwamba wamezeeka na walistahili kustaafu.

“Wapo watumishi ambao wamebadilishi umri wao wa kuishi wamebadilisha miaka yao, unakuta ni mzee kabisa lakini yeye hastaafu tu huyo naye hana utofauti sana na mfanyakazi hewa, kwa sababu ameshamaliza muda wake hataki kutoka kazini awaachie wengine nao wafanye kazi anaendelea kukaa pale kubadilisha miaka,”alisema.

“Mimi hapa nilipo nilikuwa nimebakiza miaka miwili tu kustaafu lakini hebu kaangalieni kwenye maofisi yenu wapo watu ambao ni wazee kuliko mimi bado wanafanya kazi na wanasema ndio wakati umefika, hawa nao dawa yao tunaichunguza” Rais Magufuli alisema kimsingi kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa imeenda vizuri na limefikia asilimia 98 lakini bado halijaisha.

Aliongeza kuwa katika fedha tu za watumishi hewa, ukichukulia tu mshahara serikali ilikuwa inapoteza Sh. bilioni 19.8 kwa mwezi na kwa mwaka ni zaidia Sh. Bilioni 230.


No comments:

Post a Comment