Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage leo Alhamisi amevaa viatu vya Profesa Sospeter Muhongo kwa kusoma bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni.
Mwijage anavaa viatu hivyo baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa Profesa Muhongo kama waziri wa wizara hiyo kutokana na kushindwa kusimamia vizuri wizara.
Hilo lilitokea baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya kamati ya kwanza ya kuchunguza makontena 277 ya mchanga wa madini yaliyozuiliwa kusafirishwa kugundua kuwa kuna madini mengi yanapitishwa kwenye mchanga huo.
Waziri Mwijage ambaye katika Serikali ya Awamu ya Nne aliwahi kuwa Naibu Waziri Katika Wizara ya Nishati na Madini atakuwa na kazi nzito katika bajeti hii kutokana na sakata la mchanga huo ambao wabunge wamekuwa na maoni tofauti tangu Rais Magufuli alipochukua uamuzi wa kuzuia makontena hayo.
No comments:
Post a Comment